Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli yupo mkoani Geita kwa ziara ya kikazi, ambapo leo Julai 10, 2017 anashiriki katika hafla ya makabidhiano ya nyumba hamsini za watumishi wa afya.

Nyumba hizo zitakabidhiwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa. Makabidhiano hayo yanafanyika kwa niaba ya mikoa mingine mitatu ambayo pia imejengewa nyumba hizo na Taasisi ya Benjamin Mkapa.

Pia Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida anaungana na Rais Mkapa kukabidhi mtambo wa kukamua mafuta ya alizeti. Mtambo huo umejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, kama ambavyo taarifa ilivyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa tasisi hiyo, Richard Bagolele. Tazama hapa moja kwa moja kutoka Geita muda huu

Serikali ya Kenya yatangaza amri ya kutotembea usiku
Mdee azidi kusota lupango, sakata lake lazidi kuibua mijadala