Idara ya afya katika jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini, imetangaza visa vipya 19 vya Kipindupindu ikiwa ni pamoja na vifo 10, katika mji wa Hamman-skraal.  

Idara hiyo, iliripoti kifo cha kwanza kutokana na kipindupindu Februari, 2023 baada ya wagonjwa waliokuwa na virusi hivyo, kuwasili nchini humo kutoka Malawi.

Hata hivyo, bado haijawekwa wazi ni wagonjwa wangapi wa kipindupindu waliopo nchini kote, lakini jimbo hilo la Gauteng lenye watu wengi zaidi, ambako Johannesburg na Pretoria zinapatikana, limeathirika zaidi.

Mlipuko wa mwisho wa mwisho wa ugonjwa huo nchini Afrika Kusini, ulishuhudiwa kati ya mwaka 2008 na 2009, wakati ambapo, takriban visa 12,000 viliripotiwa, kufuatia ugonjwa huo kuripotiwa nchi jirani ya Zimbabwe.

Jukwaa la Kimataifa la Uchumi: Dkt. Mwinyi awasili Doha
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 22, 2023