Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos ametaja kikosi cha awali cha timu hiyo, tayari kwa kuingia kambini kuanza maandalizi ya fainali za kombe la dunia, zitakazoanza Juni 14 nchini Urusi.

Santos ametaja kikosi cha wachezaji 35, ambacho anaamini kitakuwa na maandalizi mazuri kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho ya kukipunguza na kusalia na wachezaji 23 atakao kwenda nao nchini Urusi.

Miongoni mwa wachezaji hao, 11 walikuwepo katika fainali za 2014 zilizofanyika nchini Brazil, ambapo yupo mchezaji bora wa dunia kwa sasa Cristiano Ronaldo, Bruno Alves, Nani pamoja na William. Na wengine 19 waliunda kikosi kilichoshiriki michuano ya kombe la Mabara iliyofanyika mwaka 2017 nchini Urusi.

Wachezaji wawili katika kikosi hicho Eder na Manuel Fernandes, wanacheza ligi ya nchini Urusi katika klabu ya Lokomotiv Moscow, hivyo watakua na wakati mzuri wa kutopata changamoto za kimazingira, endapo watateuliwa kwenye kikosi cha mwisho kitakachoshiriki fainali za mwaka huu.

Kikosi kilichotajwa na kocha Fernando Santos upande wa makipa yupo Anthony Lopes (Olympique Lyonnais/France), Beto (Goztepe SK/Turkey) na Rui Patricio (Sporting CP)

Mabeki: Antunes (Getafe/Spain), Bruno Alves (Rangers/Scotland), Cedric (Southampton/England), Joao Cancelo (Internazionale/Italy), Jose Fonte (Dalian Aerbin/China PR), Luis Neto (Fenerbahce/Turkey), Mario Rui (Napoli/Italy), Nelson Semedo (Barcelona/Spain), Pepe (Besiktas/Turkey), Raphael Guerreiro (Borussia Dortmund/Germany), Ricardo (Porto), Rolando (Marseille/France), Ruben Dias (Benfica)

Viungo: Adrien Silva (Leicester City/England), Andre Gomes (Barcelona/Spain), Bernardo Silva (Manchester City/England), Bruno Fernandes (Sporting CP), Joao Mario (West Ham United/England), Joao Moutinho (Monaco/France), Manuel Fernandes (Lokomotiv Moscow/Russia), Rony Lopes (Monaco), Ruben Neves (Wolverhampton Wanderers/England), Sergio Oliveira (Porto), William (Sporting CP)

Washambuliaji: Andre Silva (AC Milan/Italy), Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Spain), Eder (Lokomotiv Moscow/Russia), Gelson Martins (Sporting CP), Goncalo Guedes (Valencia/Spain), Nani (Lazio/Italy), Paulinho (Braga), Ricardo Quaresma (Besiktas/Turkey)

Ureno wataanza kempeni ya kuusaka ubingwa wa dunia kwa kucheza dhidi ya Hispania Juni 15 katika mji wa Sochi, kisha watapambana na Morocco Juni 20 katika uwanja wa Luzhniki, na kumaliza michezo ya kundi B dhidi ya Iran, Juni 25 mjini Saransk.

Robin van Persie kusaini mkataba mpya
Video: NIDA wafunguka kuhusu tozo za vitambulisho vya uraia

Comments

comments