Nahodha na kiungo mkabaji wa Liverpool Jordan Brian Henderson atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu 2019/20 kilichosalia, kutokana na majeraha ya goti.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mpambano wa mwishoni mwa juma hili meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alisema, kiungo wake hatakuwa sehemu ya kikosi kwenye michezo yote iliyosalia msimu huu.

Liverpool Leo Jumamosi wanacheza dhidi ya Burnley, uwanja wa Anfield mjini Liverpool, huku wakiwa tayari wameshatwaa taji la Ligi Kuu ya England msimu huu 2019/20.

Henderson ambaye ni raia wa England katika msimu huu unaomalizika alikuwa kwenye kiwango bora ambapo ameisaidia Liverpool kutwaa taji la EPL baada ya miaka 30. Pia alikua sehemu ya kikosi kilichotwaa Kombe la Dunia ngazi ya vilabu.

Henderson alicheza mchezo dhidi ya Brighton ambao waliubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri, lakini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 alitolewa kufuatia majeraha ya goti yanayomkabili kwa sasa.

Klopp alesema mchezaji huyo atakuwa sehemu ya kikosi tena katika msimu mpya wa mwaka 2020/2021.

Namungo FC watangulia Fainali (ASFC)
Luc Eymael: Tunahitaji kushiriki mashindano ya CAF