Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari za kiafya kadri zitakavyotolewa na wataalam, huku akieleza kushangazwa na Watanzania walioenda nje kupata chanjo ya Corona hali iliyopelekea wao kurudi na Corona ya ajabu ajabu.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo  leo Januari 27, 2021, wakati wa uzinduzi wa shamba la miti lililopo eneo la Butengo, Chato Geita, ambalo amelipa jina la shamba la miti la Silayo, ikiwa kama sehemu ya kutambua mchango uliofanywa na Kamishna wa Mhifadhi wa Misitu nchini, Profesa Dos Santos Silayo.

“Ninajua wapo baadhi ya Watanzania wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine kwenda kuchanjwa na waliporudi wametuletea Corona ya ajabu, chanjo hazifai, wazungu wangekuwa na uwezo wa kuleta chanjo, chanjo ya UKIMWI, Malaria, Kansa na Kifua Kikuu ingekuwa imeshapatikana na kuletwa,” amesema Magufuli.

Aidha rais Magufuli aameitaika wizara ya Afya pamoja na  watanzania kuwa makini na vitu vya kuletewa toka nje ya Tanzania  na  kujiridhisha kabla ya kutumia msaada toka mataifa tajiri.

“Lazima tuwe waangalifu kwa mambo ya kuletewa letewa msije mkafikiria mnapendwa sana, Taifa hili ni tajiri, Afrika ni tajiri kila mmoja anaitamani, niiombe Wizara ya Afya, isiwe inakimbilia mambo ya chanjo bila kujiridhisha,” amesema.

Bofya hapa.

Ndayiragije: Nimewahimiza wachezaji kupambana wakati wote
Diamond aingilia kati Simba Super Cup