Mabingwa wa nchini Zimbabwe, FC Platinum wamethibitisha kumsajili mshambuliaji wao wa zamani Donald Ndombo Ngoma kama mchezaji huru.

Ngoma amekuwa hana klabu tangu aachwe na klabu ya Azam FC ya Tanzania mnamo Juni mwaka jana, na kwa muda wote huo alikua akifanya mazoezi binafsi nchini kwao Zimbabwe.

Usajili wa mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuitumikia YoungAfricans kwa mafanikio makubwa, unakuja kufuatia kuondoka kwa Perfect Chikwende aliejiunga na mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC.

Chikwende amesajiliwa Simba SC na jana Jumatano (Januari 27) alicheza mchezo wa kwanza dhidi ya Al Hilal kwenye michuano ya Simba Super Cup na kufunga bao Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es ssalaam.

Ngoma anarejea FC Platinum msimu wa 2015/16, baada ya kusajiliwa Young Africans, na sasa anarejea klabuni hapo huku aktarajiwa kutoa mchango mkubwa kwenye ligi ya Zimbabwe pamoja na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Waziri ataja njia ya kuongeza uzalishaji sukari
FIFA yabariki uchaguzi mkuu CAF