Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Manara ameonesha kusikitishwa na adhabu ya kufungiwa kwa Afisa Habari wa Young Africans Hassan Bumbuli, iliyotolewa jana jioni na kamati ya maadili na nidhamu za Shirikisho la soka nchini TFF.

Bumbuli amefungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitatu, kufuatia kukaidi kulipa faini ya shilingi milioni tano, baada ya kukutwa na hatia ya kusema uongo juu ya sakata la kiungo mshambuliaji wa Simba SC Bernard Morrison.

Manara ameonesha masikitiko hayo kupitia taarifa aliyoiandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, ambapo amekiri alitamani kuona Bumbuli akiendelea kuwa sehemu ya soka la Tanzania.

Manara ameandika: Nilitamani uendelee kuwa nami ktk kazi hii kubwa ya kuusemea mpira wetu na kuendelea kuupromot ila bad luck haipo hvyo!!

Hatujawahi kuwa marafiki ila wote tunafanya kazi ya aina moja ingawa tunatofautiana uwezo na maarifa!!

Najua uliwahi kunitolea matusi machafu hadharani, Najua uliingia kwa mbwembwe nyingi na kusema mimi sio mweledi na nyie mtaleta weledi mpya katika usemaji wa soka nchini,Lakini Imani ya dini yangu inaniambia nisamehe na nilishakusamehe bro!!

Ninalokuomba tulia na rejea kuziomba mamlaka zifanye reiview kwa kesi yako kisha lipa fine uliyopigwa na nipo tayari kutoa pesa yote uliyopigwa faini ili maisha mengine yaendeleee !!

I feel sorry for you na inshaallah utarejea katika soka @hbumbuli

Mtibwa Sugar yatuma salamu Ligi Kuu
Waziri ataja njia ya kuongeza uzalishaji sukari