Baada ya kuadhibiwa na Shiriksho la soka nchini TFF kupitia kamati za Maadili na Nidhamu kwa kufungiwa miaka mitatu kujihusisha na masual ya soka, Afisa habari wa Young Africans Hassan Bumbuli ametoa kauli kwa mara ya kwanza.

Bumbuli amekiri kusikia na kupokea barua inayomuarifu juu ya kuadhibiwa kwake, lakini amesema hajaridhishwa na maamuzi yaliyochukuliwa dhidi yake, hivyo amejipanga kuchukua hatua ambayo huenda ikamuondolewa adhabu kama si kupunguziwa kifungo.

Bumbuli amesema: “Adhabu nimeiona na tumeipokea. Kama uongozi kwanza hatujaridhika, hiyo ni hatua ya kwanza, hatua ya pili itafuata kwa sababu kuna nafasi ya kukata rufaa na tutakata rufaa.”

“Nililipa faini na pay slip nilipeleka TFF ikapokelewa na mhasibu, kwa bahati mbaya akasema hakuwa na risiti kwa muda ule kwa hiyo risiti nitaifata. Sisi copy za pay slip tunazo.”

“Wote walikuwa na taarifa kuanzia wanasheria wa TFF, tukaenda kwenye Kamati nikawaambia kila kitu kwa hiyo kila mmoja alikuwa anataarifa hiyo pesa imeshalipwa. Hilo suala la kukaidi halikuwepo, tulikuwa tumedhamiria kukata rufaa lakini kwa bahati mbaya hatukupewa vitu tulivyokuwa tunavihitaji kwa ajili ya kukata rufaa kwa wakati ambao tulikuwa tunahitaji.”

“Hukumu haikuonesha chochote kwamba natakiwa kulipa faini ndani ya muda gani, barua ilieleza kwamba natakiwa kulipa faini, sitakiwi kufanya kosa la kimaadili ndani ya miaka miwili na nina haki ya kukata rufaa”

Ushangiliaji wa Morrison wamkera Masau Bwire
Mostafa Mohamed kutimkia Galatasaray