Aliyekuwa nahodha na Mlinzi wa kushoto wa kikosi cha Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’ Laurian Mpalile ametangaza kustaafu kucheza soka la ushindani.

Mpalile ametangaza uamuzi huo, huku akiwaweka rekodi ya kipekee ndani ya klabu hiyo, ambayo imehamishia maskani yake mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, ikitokea Jijini Mbeya.

Rekodi iliyowekwa na beki huyo, ni kuwa mchezaji pekee wa Tanzania Prisons aliecheza kwa muda mrefu zaidi, akifanya hivyo tangu mwaka msimu wa mwaka 2006/07 hadi 2020/21.

Kwa kipindi chote hicho Mpalile hakuwahi kuihama Tanzania Prisons wala kujihusisha na matamanio ya kwenda kwenye klabu tofauti na Maafande hao, hadi ametangaza kustaafu.

Hata hivyo Mpalile alikua sehemu ya kikosi cha Tanzania Prisons kilichosajiliwa msimu huu 2020/21, hivyo kutangaza kwake kustaafu soka huenda ikiwa nafasi kwa uongozi wa Tanzania Prisons kumpandisha mchezaji mwingine kutoka kikosi cha vijana ndani ya klabu hiyo atakaeziba nafasi yake.

Mpalile anaiacha Tanzania Prisons ikiwa kwenye nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kushika dimbani mara kumi na nane.

Prisons imepoteza michezo sita, huku ikishinda michezo mitano na kupoteza michezo saba ndani ya msimu huu, ambao tayari umeshaingia kwenye mzunguuko wa Pili.

KILA KHEIR LAURIAN MPALILE

Rais Magufuli aagiza Madaktari waliohama watafutwe
Ndayiragije ajitetea Stars kutolewa 'CHAN'