Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linafuatilia kifo cha dereva wa lori mkazi wa Tunduma mkoani Songwe kilichotokea jana Alhamisi Januari 28, 2021 muda mfupi baada ya polisi kukamata  lori hilo.

Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha askari polisi takribani wanne wakiwa wamelizunguka lori hilo na mmoja akimvuta dereva huyo ili ashuke na alipofanikiwa, wote walimbeba na kumweka kando ya barabara huku dereva huyo akionekana kukosa nguvu.

Akizungumza na  Mwananchi Digital leo Ijumaa Januari 29, 2021 kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Jeromr Ngowi amekiri kutokea kwa tukio hilo, akisisitiza kuwa atatoa ufafanuzi baada ya kufika eneo la tukio na kupewa taarifa sahihi.

“Kwa sasa niko eneo la tukio nataka kujiridhisha na nitatoa taarifa wa vyombo vya habari kuhusu  tukio hili,” amesisitiza.

Waziri awaonya watakao chezea miradi ya maji
Ushangiliaji wa Morrison wamkera Masau Bwire