Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, ametangaza siku saba za kupiga nyungu kwa Watanzania huku wakiendelea kumuomba Mungu Kuzima kuenea kwa virusi vya Corona.

kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 30, 2021, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tabora mara baada ya Rais Dkt. John Magufuli, kumaliza kuweka jiwe la msingi katika jengo la wagonjwa wa dharura katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora pamoja kuzindua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda maeneo ya Tabora, Nzega na Igunga.

Jafo mesema kuwa zoezi hilo la kujifukiza amelipa jina la ‘One week season Three’ ili watu wajifukize huku wakiendelea kuchapa kazi na Corona ikose nafasi.

Marufuku uagizwaji wa nyuzi za kufungia tumbaku

“Hapa Corona haina nafasi, Mh Rais tutaendelea kumuomba Mungu kama ulivyoelekeza na umesema watu wajifukize sana na Rais naomba nikuambie Jumatatu tunaanza kampeni nyingine ya one week season three, nyungu kama kawaida tunajifukiza, tunakula matunda tunaanza tarehe 1 hadi tarehe 7 hatupoi kazi inaendelea, uchumi wetu lazima usimame”, amesema Waziri Jafo.

Magufuli anyooshea kidole migogoro ya ardhi Singinda
Magufuli awachana viongozi Tabora ' jengeni umoja sio majungu'