Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema itasimamisha mpango wake wa kuwapa chanjo dhidi ya COVID-19 wafungwa wa makosa ya ugaidi wanaoshikiliwa kwenye kambi ya Guantanamo kufuatia kuongezeka kwa malalamiko wakati ambapo nchi inatoa chanjo kwanza kwa watumishi wa afya na wazee.

Msemaji wa wizara hiyo, John Kirby, ameandika hayo kupitia ukurasa wa Twitter akisema hakuna mfungwa yoyote kwenye kambi hiyo ambaye tayari amechanjwa.

Kirby amekiri akisema ni kweli Rais Joe Biden amesema ana mpango wa kutokomeza virusi vya corona katika siku yake ya kwanza ofisini lakini hakusema atawapa chanjo magaidi kwanza kabla ya Wamarekani.

Kambi ya Guantanamo iliyoko Cuba inawashikilia washukiwa wa makosa ya ugaidi ikiwa ni pamoja na Khalid Sheikh Mohammed, mfuasi wa kundi la Al-Qaeda anayedaiwa kupanga shambulizi la Septemba.

Kiswahili champandisha cheo Jaji
Magufuli anyooshea kidole migogoro ya ardhi Singinda