Maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa leo mishale ya saa moja jioni Uwanja wa Azam Complex Chamazi, kati ya Azam FC dhidi ya Mabingwa wa Soka DR Congo TP Mazembe yamekamilika.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC, Zakaria Thabit ‘ZakaZakazi’  amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na wanaamini watapata matokeo mazuri pamoja na kuimarisha kikosi chao.

Thabit amesema anaamini kikosi chao kitaweka histoaria ya kuwafunga TP MAzembe ndani ya dakika 90, baada ya klabu za Simba na Young Africans kushindwa kufanya hivyo.

“Kwa timu za Tanzania, ni Azam FC pekee ambayo imeweza kuifunga TP Mazembe ndani ya dakika 90 uwanjani hivyo unaona kwamba rekodi zetu sisi zipo vizuri.”

“Julai 16, 2019 kwenye robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame nchini Rwanda, Azam FC tulishinda kwa mabao 2-1.”

“Mabao ya Azam FC yaliwekwa kimiani na winga Idd Seleman ‘Nado’ na mshambuliaji Obrey Chirwa, huku lile la Mazembe likifungwa na Ipamy Giovani. Hapo unaona namna gani tupo vizuri.”

“Licha ya kwamba ni mchezo wa kirafiki wachezaji wetu watapambana ili kupata matokeo mazuri na itakuwa ni sehemu ya kazi kwa ajili ya kuelekea kwenye mechi za ligi pamoja na mashindano mengine.” Amesema Thabit.

Azam FC imetumia fursa ya ujio wa TP Mazembe hapa nchini kucheza mchezo huo wa kirafiki, baada ya kumalizika kwa michuano ya Simba Super Cup mwishoni mwa juma lililopita.

Katika michuano ya Simba Super Cup, TP Mazembe ilicheza dhidi ya Al Hilal ya Sudan na kuambulia kichapo cha mabo mawili kwa moja kisha ikambulia sare ya bila kufungana dhidi ya  Mabingwa Tanzania Bara Simba SC.

Halima Mdee na wenzake kushiriki kikao cha Bunge Leo
Bunge la 12 laanza bila kambi ya upinzani