Imeelezwa kuwa wachezaji wa Simba jana Jumatatu (Februari Mosi) walihitaji kikao na nyota wa kikosi hicho, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Licha ya kulipia faini na kuomba msamaha bado imekuwa ngumu kwa nyota huyo kurudi Simba baada ya wachezaji kugomea uongozi kurejea kwa  nyota huyo mpaka pale watakapokaa naye kikao.

“Wachezaji wamegomea Mkude kurudi kambini kwa sasa na wameshikilia msimamo kwamba ikiwa atarudi mazoezini bila ya kufanya naye kikao basi watamuacha afanye mazoezi peke yake, wao wataendelea na mambo mengine.”

“Kutokana na msimamo huo sasa uongozi umewaambia wachezaji kwamba wapange siku ya kuzungumza na Mkude ambapo kesho (leo) watakaa naye, wakimalizana basi atarejea kikosini kuendelea na mazoezi.” kilielezea chanzo hicho.

Tangu asimamishwe mpaka sasa Mkude amekosa michezo minane ambazo Simba wamecheza za michuano yote hivyo amebakiza michezo miwili kabla ya kurejeshwa rasmi.

Julio alia na wachezaji Stars, ataka wajiongeze
Halima Mdee na wenzake kushiriki kikao cha Bunge Leo