Mabingwa wa soka nchini England Liverpool FC wataikosa huduma ya beki wa kati kutoka nchini Cameroon Job Joël André Matip, hadi mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa za beki huyo mwenye umri wa miaka 29 kuwa nje hadi mwishoni mwa msimu huu, zimetolewa na jopo la madaktari wa klabu hiyo, baada ya kuumia akiwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tottenham Hotspurs uliochezwa Janauri 28.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amekiri kupokea taarifa za kukosekana kwa Matip kwa masikitiko makubwa, hasa ikizingatiwa mabeki wake mahiri Van Djik pamoja na Joe Gomez nao ni majeruhui.

“Matip atakuwa tayari kurejea uwanjani wakati wa kujiandaa na msimu ujao, kila kitu kitakua sawa.” Amesema Klopp

Hata hivyo tayari klabu ya Liverpool imeshafanya usajili wa wachezaji wanaocheza nafasi ya ulinzi Ben Davies na Ozan Kabaki ambao wataziba nafasi za Joel Matip, Van Djik pamoja na Joe Gomez.

Uganda: Jeshi lakemea ujumbe wa vitisho ulioenea mitandaoni
Kumbe Simba SC walitaka kumsajili Fiston wa Young Africans