Kiungo wa kimataifa wa Tanzania Himid Mao Mkami “Ninja” amekamilisha hatua za kujiunga na klabu nyingine ya Ligi kuu nchini Misri Entag El-Harby SC akiachana na ENPPI.

Himid mwenye umri wa miaka 28, amejiunga na klabu hiyo akiwa mchezaji huru, kufuatia mkataba wake na klabu ya ENPPI kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita.

Himid anakuwa mchezaji wanne kusajiliwa na Entag El-Harby SC akitanguliwa na Ahmed Saber pia kutoka ENPPI, Mohamed Sosta kutoka Aswan, na mlinda mlango Ahmed Busca.

Klabu ya Entag El-Harby SC imekua na mwanzo mbaya katika msimu huu wa Ligi ya Misri, hali iliyopelekea kuburuza mkia wamsimamo wa ligi hiyo, ikiwa na alama tano tu, baada ya kucheza michezo tisa.

Mtiririko wa matokeo mabaya ulisababishwa kutimuliwa kwa kocha Mokhtar Mokhtar, ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Hamada Sedky.

Usajili wa kina Himid Mao ‘Ninja’ ni sehemu ya kuboresha kikosi cha Entag El-Harby SC, na inaaminiwa wataweza kurejea kwenye makali ya kushindana na klabu nyingine zinzoshiriki Ligi Kuu ya Misri.

Himid Mao alianza kucheza soka nchini Misri Julai 2018, akisajiliwa na Petrojet, lakini mwaka mmoja baadaye alihamia ENPPI, akiichezea michezo 22 msimu uliopita.

Kwa ujumla, kiungo huyo mwenye sifa kubwa ya kukaba ana michezo 54 nchini Misri, akifunga mabao matatu na kutoa Assist moja kwa Petrojet na ENPPI.

Twitter yafungia akaunti za wanaharakati wa kilimo
Wizara ya Kilimo yaja na huduma mpya