Hatimaye Mshambuliaji Lionel Messi amejifuta machozi ya muda mrefu kwa kutwaa taji la Copa America akiwa na timubyake ya taifa kwa mara kwanza.

Messi alikuwa na wakati mgumu miaka nenda rudi tangu alipoanza kuitumikia timu ya taifa ya wakubwa ya Argentina kwa kukosa mataji.

Ameshuhudia akicheza Fainali nne (Tatu za Copa America na moja ya Kombe la Dunua) bila kuwa na furaha.

Leo alfajiri gwiji huyu wa FC Barcelona alimaliza mchezo wa Fainali akiwa na kicheko, baada ya Argentina kuibanjua Brazil bao 1-0 katika ardhi ya nyumbani kwao Rio de Janairo.

Bao liliofungwa na Mshambuliaji wa klabu yaa PSG Angel Di Maria lilitosha kuwapa Argentina kicheko cha ubingwa wa Copa America kwa mwaka 2021.

Kwa mantiki hiyo Brazil waliokua Mabingwa watetezi, wameutema ubingwa wao mikononi mwa wapinzani wao wa jadi katika ukanda wa America ya Kusini.

Siri nzito zilizotunzwa kikosi cha Argentina
Ukweli kuhusu moto kuunguza Soko la Kariakoo, Mkuu wa Mkoa azungumza