Mwanamitindo na mjasiriamali maarufu Duniani Kim Kardashian amejikuta akishindwa kuendelea kuificha siri ya mahusiano yake na nyota wa Sanaa ya uchekeshaji Pete Davidson.

Baada ya kuenea kwa tetesi zilizoambatana na picha za wawili hao kuwa ni wapenzi, hatimaye wameamua kuthibisha rasmi kuwa kwenye uhusiano kwa kuamua kuwa huru kuonekana hadharani.

Kwa mujibu wa Daily Mail inaelezwa wawili hao walionekana pamoja wakiwa katika matembezi huko Palm Springs California nchini Marekani, huku mienendo ya kimahaba baina yao ikiwa imetawala.

Baadhi ya picha zilizonaswa zinawaonyesha wakiwa wameshikana mikono kwa namna inayothibisha kuwa kwa sasa hakuna Siri tena.

Si muda mrefu sana tangu tetesi za Kim Kardashian na Pete kutoka kimapenzi kuanza kuenea kote mitandaoni, ambapo mengi yaliibuka zaidi baada ya kipindi cha “SNL SKIT” takriban mwezi mmoja uliopita siku ambayo Kim Kardashian alialikwa na kuwa Host.

Baada ya Kim na Pete kuoneka kwa mara ya kwanza kupitia ‘SNL SKIT’ ripoti kadhaa ziliendelea kuarifu kuwa wawili hao walikuwa wakionekana sehemu mbali mbali za kula bata.

Kim Kardashian anaingia kwenye uhusiano mpya punde baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake rapa Kanye west waliofunga ndoa Mei 24, 2014 na kubarikiwa kupata watoto wa nne North 8, Psalm, 2, Chicago na Saint.

Breaking news: Hotel ya Villa de Coco inaungua
Hiki kimekuja wakati muafaka - Makalla