Habari kutoka Somalia zinasema kuwa watu 18 wameuawa baada ya bomu kulipuka na kuharibu kabisa basi walilokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba abiria wote waliouawa katika ajali hiiyo walikuwa raia.

Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa karibu wa Lafole.

Inadhaniwa kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi lililokuwa karibu.

Mara kwa mara wapiganaji wa Al Shaabab hulenga wanajeshi wa Serikali, na huu utakuwa ni muendelezo wa matukio ya ushambuliaji yanayofanywa  na wanamgambo hao sehemu mbali mbali.

N’Golo Kanté Atengewa Pauni Milioni 25
Ryan Giggs Akataa Kufanya Kazi Na Jose Mourinho