Obama kuja na msafara wa watu 700

By dar24.com - Fri May 24, 6:08 am

Obama_0c245_image_1024w1

Rais wa Marekani, Barrack Obama anatarajiwa kuwasili na msafara wa watu 700 katika ziara yake katika nchi ya Tanzania. Rais Obama anatarajia kuwasili na msafara watu 700 Julai mosi. Kufuatia hilo  baadhi ya hoteli zenye hadhi ya nyota tano jijini Dar es Salaam zimeanza kusitisha kupokea wageni kutokana na ujio huo.

aarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani ilisema Rais huyo, anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi kwa ajili ya ziara ya siku tatu hadi Julai 3 mwaka huu ili kuimarisha uhusiano baina ya nchi hiyo pamoja na nchi za Afrika. Msafara huo utajumuisha watu mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara.

Akizungumzia ziara hiyo jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema tayari timu ya kwanza imewasili nchini kwa ajili ya maandalizi mbalimbali.

“Ni ujio mkubwa na atakapokuwa nchini atazungumzia masuala mengi ikiwamo namna ya kuiwezesha Afrika kuwa na umeme wa kutosha kwa sababu ukiwa nao maendeleo yanakuwa mazuri,”alisema Membe.

Hoteli zasitisha upokeaji wageni

Gazeti hili lilifanya uchunguzi katika hoteli mbalimbali zenye hadhi ya nyota tano ambazo mara nyingi viongozi wakuu wa nchi mbalimbali huzitumia pindi wanapofika nchini. Hoteli hizo zilizoko katikati ya jiji zimechukuliwa kuanzia Juni Mosi hadi Julai 5.

Uchunguzi huo umebaini kuwa,wageni waliochukua nafasi katika hoteli hizo wataanza kufika kati ya Juni 25 na kuondoka Julai 5.

Mpaka sasa hali ya usalama katika hoteli hizo umeimarishwa ili kuhakikisha kuwa wateja wanaowasili katika maeneo hayo wanaishi katika mazingira salama.

No tags for this post.

Leave a Reply

Switch to our mobile site