KIKOSI cha Mbeya City Fc  kesho jumapili kinashuka kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, kucheza mchezo wa kufungia msimu  wa 2015/16 katika ligi kuu ya soka Tanzania  bara dhidi ya wageni Ndanda Fc kutoka mkoani Mtwara.

Muda  mfupi uliopita meneja  wa kikosi cha City, Geoffrey Katepa  amedokeza kuwa  nyota wote 18 wameandaliwa kwa ajaili ya kuwakilisha  timu yao na wako katika hari nzuri, tayari kusaka ushindi.

DSC_0101

“Kama unavyoona  tumemaliza mazoezi  muda huu, yalikuwa ni mazoezi mepesi kueleka  mchezo wa kesho kila mmoja yuko vizuri na ana ari kubwa, jambo muhimu kwetu ni kushinda mchezo huo ili tumalize ligi kwa heshima, hatuna wasiwasi wowote tuko salama kwenye msimamo wa ligi, kumaliza kwa ushindi kutatuweka kwenye mapumziko mazuri  kwa matayarisho ya msimu mpya”, alisema.

Kuhusu  majeruhi Katepa  alisema kuwa City itakosa huduma ya nahodha na mlinzi shupavu wa kushoto Hassan Mwasapili alaiye majeruhi kufuatia maaumivu ya nyama za paja  yanayomkabili, pia  Temi Felix na Deo Julius  hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho kupisha majeraha waliyonayo.

 

Ulevi wa Kitwanga ulivyowanyima Ukawa ‘pointi 3 muhimu’
Pazia Ligi Kuu Ya Vodacom Msimu Wa 2015-16 Kufungwa Rasmi