Mahakama ya jijini Cairo nchini Misri imewahukumu kifo watu 21 kwa kosa la kujihusisha na ugaidi kwa nyakati tofauti.

Watu hao walikutwa na hatia ya kujiunga na makundi ya kigaidi na kupanga mashambulizi dhidi ya watu wasio na hatia, majengo ya sekta binafsi na sekta ya umma. Wanadaiwa pia kupanga kuwaua askari wa jeshi la polisi na jeshi linalolinda mipaka ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Misri, watu hao wanadaiwa pia kupanga kufanya mashambulizi ya mabomu katika vituo vya polisi katika Pwani ya jiji la Damietta pamoja na bomba la gesi katika kijiji cha jirani.

Hukumu ya mwisho ilipitishwa na mahakama ya nchi hiyo na baadaye kupitishwa na kiongozi mkuu wa kidini nchini humo (Grand Mufti), Sheikh Shawki Allam.

Wafanyakazi wa ndani waandamana kudai haki zao

Utafiti wazitaja nchi zinazoongoza kwa rushwa sekta ya umma

Baadhi ya watuhumiwa hawakuwa mahakamani wakati hukumu dhidi yao ilipokuwa inasomwa.

 

Kigogo CRDB ahukumiwa jela miaka 93
Wafanyakazi wa ndani waandamana kudai haki zao