Wizara ya Afya nchini, inaendea na juhudi za ugawaji wa Dawa na matibabu kwa wagonjwa wenye maradhi yasiyopewa kipaumbele, ili kuweza kutokomeza magonjwa hayo hayo ifikapo mwaka 2030.

Meneja Mpango Wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Dkt. George Kabona ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumzia Kampeni na mkakati wa kutokomeza magonjwa hayo.

Amesema, “katika wiki hili la magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele huduma zinaendelea kutolewa katika mikoa ya Mkoa wa Tanga, Dodoma na Arusha na Tanzania tunaadhimisha kwa utoaji wa huduma ya upasuaji wa Mabusha.”

Kwa upande wake Afisa Mpango wa Taifa Wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Oscar Kaitaba amesema Ugonjwa wa matende na mabusha hauna uhusiano wowote na ulaji wa madafu, bali huenezwa na Mbu wa aina zote.

Hamis Juma Mbizo 'H-Mbizo' afariki Dunia
Coastal Union yamkana Julio