Umoja wa Mataifa UN umesema zaidi ya asilimia 50 ya dawa zinazopatikana katika eneo la Afrika ya magharibi zimetajwa kutokidhi vigezo vinavyostahili au bandia na suala hilo limeainishwa katika ripoti yake ya biashara haramu ya bidhaa za matibabu.

UN kupitia taarifa yake imeeleza kuwa, biashara hiyo inaweza kusababisha dawa za kuua wadudu kutofanya kazi, maambukizi ya magonjwa hatari, huku pia ikidhoofisha umaanifu katika mifumo ya afya.

Ofisi ya Umoja wa mataifa kuhusu dawa za kulevya na uhalifu (UNODC), imesema kati ya Januari 2017 na Disemba 2021, takriban tani 605 ya bidhaa za matibabu zilikamatwa Afrika magharibi, wakati wa operesheni za kimataifa.

Aidha, ripoti hiyo imezidi kufafanua kuwa, zaidi dola milioni 44.7 zinatumiwa kila mwaka kutibu watu waliotumia dawa bandia za malaria na hali hiyo imesababisha vifo 267,000 vinavyohusishwa kila mwaka na matumizi ya dawa hizo.

Rais Samia ataja mikakati urekebishaji mifumo ya haki
EWURA yatangaza ukomo wa bei ya mafuta