Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambaye ni Mbunge wa Namtumbo Mhandisi Edwin Ngonyani amekanusha habari iliyochapishwa kwenye gazeti la Mseto kuwa si za kweli na ina lengo la kumchafua katika utendaji wake wa kazi.

Amesema hayo mapema hii leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari,Mhandisi Ngonyani amesema kuwa taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye gazeti la Mseto la tarehe 4 Agosti 2016 ikiwa kwenye ukurasa wa kwanza yenye kichwa cha habari kilichoandikwa “WAZIRI AMCHAFUA JPM”.

Habari hiyo ikiwa na nukuu “Waziri wa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kudaiwa kupokea fedha za kufanyia kampeni za ubunge kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa kuwaahidi kuwa mitaji yao nchini itakuwa salama”. 

Aidha Mhandisi Ngonyani amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuandika habari zenye taarifa kamili na kweli ili kuepuka upotoshwaji.

Habari hiyo ilikuwa imedai kuwa Mbunge huyo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amepokea kiasi cha dolla elfu 65 kwa Bw. James Sinclair ili zimsaidie kupata nafasi ya ubunge.

Imeongeza kuwa alipewa kiasi cha dolla elfu 25 kutoka kwa Dr. Alphonce Koigi Machari ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trans Century ili apate nafasi hiyo hiyo ya ubunge.

Mhandisi Ngonyani amelitaka gazeti hilo kukanusha taarifa hiyo kwa haraka iwezekanavyo

Ni Real Madrid Tena, Waigaragaza Sevilla CF
Tasaf Kunufaisha Kaya Masikini Ilala