Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa ameteua kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya kambi maalum ya kujiandaa na pambano la kukamilisha ratiba ya mbio za kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria.

Vijana wamepewa nafasi kubwa katika kikosi cha Mkwasa huku kiungo wa Mtibwa Sugar Ibrahim Jeba akiitwa kwa mara y kwanza.

Joseph Mahundi wa Mbeya City na Jamal Mnyate aliyehamia Simba pia wameitwa kwa mara ya kwanza.

Kikosi Kamili:

Walinda Milango: Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benno Kakolanya.

Walinzi: Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Mohamed Hussein, Juma Abdul, Erasto Nyoni.

Viungo: Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Hassan Kabunda, Simon Msuva.

Washambuliaji: Joseph Makundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Hajib, John Bocco, Jeremiah Juma.

Diwani Ilala Atoa Wito Kwa Serikali na Mashirika Kusaidia Dar Festival
Video: Pesa ninazozipata ni nyingi kuliko Ubunge - JB