Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza orodha ya wachezaji 40 ambao wataingia kwenye mchakato wa kuunda kikosi bora cha mwaka.

Katika orodha hiyo hakuna mchezaji yoyote kutoka nchini England, Ireland na Scotland lakini imekua bahati kwa wachezaji kutoka nchini Wales.

Wales imetoa watatu katika orodha hiyo ambao ni Joe Allen, Gareth Bale pamoja na Aaron Ramsey.

Orodha hiyo ya UEFA itawashirikisha mashabiki wa soka duniani ili kuweza kukichagua kikosi bora cha mwaka, na utaratibu huo umekua ukifanyika kwa kipindi cha miaka 16 iliyopita.

Orodha iliyotolewa ina walinda milango 4, mabeki 12, viungo 12 na washambuliaji 12.

Kikosi cha wachezaji 40 ambacho kitapigiwa kura na mashabiki:

MAKIPA: Gigi Buffon (Juventus), Keylor Navas (Real Madrid), Jan Oblak (Atletico Madrid), Rui Patricio (Sporting).

MABEKI: Toby Alderweireld (Tottenham), Jerome Boateng (Bayern Munich), Leonardo Bonucci (Juventus), Dani Carvajal (Real Madrid), Diego Godin (Atletico Madrid), Raphael Guerreiro (Borussia Dortmund), Juanfran (Atletico Madrid), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Laurent Koscielny (Arsenal), Pepe (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid).

VIUNGO: Joe Allen (Stoke), Yannick Carrasco (Atletico Madrid), Kevin De Bruyne (Man City), Andres Iniesta (Barcelona), N’Golo Kante (Chelsea), Toni Kroos (Real Madrid), Grzegorz Krychowiak (PSG), Riyad Mahrez (Leicester), Luka Modric (Real Madrid), Dimitri Payet (West Ham), Paul Pogba (Manchester United), Aaron Ramsey (Arsenal).

WASHAMBULIAJI: Sergio Aguero (Man City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth Bale (Real Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gonzalo Higuain (Juventus), Zlatan Ibrahimovic (Man United), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Lionel Messi (Barcelona), Neymar (Barcelona), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Alexis Sanchez (Arsenal), Luis Suarez (Barcelona).

Orodha Ya Wanaowania Tuzo Ya Bao Bora 2016
Yametimia, Hector Bellerin Kubaki Arsenal FC