Wakati Brazil ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa Copa America nahodha wa timu ya taifa hilo, Dani Alves ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuchukua mataji mengi katika historia ya mchezo wa mpira wa miguu tangu kuanzishwa kwake hadi sasa.

Alves ameweka rekodi hiyo ya kubeba mataji 40 katika maisha yake ya Soka baada ya kuingoza timu yake ya taifa katika mchezo wa fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya timu ya taifa ya Peru mtanange ambao ulipigwa kwenye dimba la Maracana ambapo Brazil waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 kuweza kunyakua taji hilo kwa mara ya tisa.

Yafuatayo ni mataji ya awali ambayo amewahi kuyabeba mchezaji huyo wakati akiwa kwenye vilabu mbalimbali alivyo pitia pamoja na mataji ya timu ya taifa

Wakati akiwa Sevilla

Uefa cup x 2

Uefa super cup x 1

Kombe la mfalme x 1

Super copa x 1

Wakati akiwa Barcelona

La liga x 6

Kombe la mfalme x 4

Super copa x 4

UEFA x 3

Kombe la dunia la klabu x 3

UEFA super cup x 3

Wakati akiwa Juventus

Kombe la ligi kuu ya Italia Sereia A x 1

Coppa Italia x 1

Mataji ya klabu yake ya sasa ya Paris Sant Germany

Kombe la ligi kuu nchini humo, Leagua 1 x 2

Trophee de champion x 2

Coupe de La league x 1

Coupe de France x 1

Mataji aliyo beba na timu yake ya taifa ya Brazil

Copa America x 2

Confederations Cup x 2

Pia mchezaji huyo mwenye miaka 36 alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo ambayo imefanyika nchini humo ambapo ni mara yake ya pili kunyakua taji hilo akiwa na timu  yake hiyo lakini ni mara yake ya kwanza akiwa kama nahodha ambaye aliteuliwa na koch amkuu wa timu hiyo Adenor Leonardo Bacchi almaarufu Tite.

Timu ya taifa ya Marekani yatwaa ubingwa wa Wanawake
Video: Msaidizi wa Membe adaiwa kutekwa Dar | Askofu afunguka kuhusu utekaji

Comments

comments