Shirika la kutetea haki za binadamu, la Iran (IHR), limesema kiasi watu 448 waliuawa na vikosi vya usalama nchini Iran katika harakati za kuyakabili maandamano yaliyoanza katikati ya mwezi Septemba, 2022.

Shirika hilo limesema, nusu ya watu hao (224), wameuwawa katika maeneo ya jamii za makabila ya waliowachache tangu kuanza kwa maandamano hayo.

Waandamanaji katika moja ya matukio nchini Iran. Picha ya Jordan Times

Shirika hilo, lenye makao yake nchini Norway, kati ya watu hao 448 waliouliwa 60 walikuwa ni watoto chini ya umri wa miaka 18 wakiwemo wasichana tisa na wanawake 29.

Awali, Brigedia jenerali. Amirali Hajizadeh kutoka jeshi la kimapinduzi la jamhuri hiyo ya kiislamu alisema zaidi ya watu 300 waliuawa, ikiwa ni kauli ya kwanza ya mamlaka kukiri kuhusu idadi ya waliouwawa.

Uharibifu Ukraine: Urusi yakalia kuti kavu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 30, 2022