Beyonce Knowles amezua jambo kwa mashabiki wake baada ya kuweka picha mpya kwenye mtandao, picha ambazo zimewafanya baadhi ya watu kudai kuwa tayari ameshajifungua mapacha wake kimyakimya.

Picha hizo zinazomuonesha yeye na mwanae wa kike Blue Ivy, inaonesha umbo lake hususan tumbo limepungua. Hivyo, watu mashabiki walidai kuwa kama ilivyo kawaida yake ya usiri na kutofanya mahojiano kwa muda mrefu, ameamua kutoa ujumbe kwa picha.

Hali iliyochochea tetesi hizo ni pale mama yake mzazi, Tina alipoonekana katika hospitali moja jijini Los Angeles hivi karibuni. Wakati huohuo mdogo wake, Solange aliahirisha tamasha lake Boston.

“Natabiri Beyonce ameshajifungua na hakuna anayejua. Solange aliahirisha ghafla tamasha lake la Boston. Ni dhahiri B amejifungua,” zinasomeka moja kati ya tweets maarufu zilizoibua mjadala huo.

Familia ya Beyonce na Jay – Z inajulikana zaidi kwa usiri, na hata wakati wa kujifungua Blue Ivy ulifanyika usiri mkubwa ikiwa ni pamoja na kuficha hosptali husika kwa muda.

Majaliwa aitaka Halmashauri ya Kilosa kulipa deni kabla juni haijaisha
Black eyed peas kupamba fainali za UEFA champion league