Rapa 50 Cent, ambaye anatajwa kuwa ‘kombora’ lisilotabirika litatua wapi wowote, ametua kwa Ashanti ambaye ni swahiba wa muda mrefu wa hasimu wake, Ja Rule baada ya kuripotiwa kuwa ameuza tiketi 24 tu za tamasha lake.

Tamasha la Ashanti liliripotiwa kuahirishwa baada ya tiketi zake ‘kudoda’ kwenye Chuo Kikuu cha Stonny Brook.

50 aliweka kwenye Instagram picha ya Ja Rule akiwa na Ashanti pamoja na habari hiyo, akirusha kombora kuwa amekuwa akiwatahadharisha watu kufanya kazi na Ja Rule.

“Tamasha la Ashanti limefutwa baada ya kuuza tiketi 24. Subiri kidogo, nadhani nilimwambia kila mtu asijihusishe na huyu mjinga. Ninahitaji majina ya kila mtu aliyenunua tiketi sasa hivi,” tafsiri isiyo rasmi ya alichokiandika, akimaliza na msemo wake maarufu ‘Get the Strap’.

Ashanti na Ja Rule ambao walikuwa wanatamba muda mrefu na kutawala chati mbalimbali za muziki, hivi karibuni wameachia wimbo wa pamoja unaoitwa ‘Encore’.

Wakizungumzia sababu za kuahirisha tamasha hilo, waandaaji wa tamasha hilo waliweka wazi kuwa lengo lao lilikuwa kuhakikisha wanafunzi wanapata burudani lakini mambo yalienda kombo baada ya kuona wameuza tiketi 24 tu.

Lema aeleza alichoulizwa Polisi kuhusu Mo Dewji kutekwa
Makamba aeleza alivyohojiwa sakata la Mo Dewji, ‘sikukamatwa’

Comments

comments