Rapa 50 Cent alimanusura amchape makofi msanii chipukizi aliyemfuata na kumsimamisha barabarani wakati akiwa kwenye matembezi ya jioni na binti mmoja bila walinzi wake.

Video iliyosambaa mtandaoni imemuonesha rapa huyo akiwa kwenye majibizano na msanii mchanga aliyejulikana kwa jina la NFL dume ambaye alimtaka 50 Cent amuunge mkono  na angalau aitizame ukurasa wake wa Instagram

Hata hivyo 50 Cent alichomoa ombi hilo kwa madai kuwa hajatembea na walinzi wake hivyo ni hatari kwa usalama wake kukutana na watu

Rapa 50 Cent alimwambia kijana huyo kuwa yupo hapo kwaajili ya mtoko na binti mrembo ambae alionekana pembeni lakini kauli hiyo haikumuingia kijana huyo na kuzidi kumzonga 50 Cent

Baada ya kuona msanii haelewi 50 Cent alitaka kumkunja lakini baada yakugundua eneo hilo lina kamera iliyokuwepo pembeni yake alisita kufanya maamuzi magumu.

Msipowekeza kwenye maeneo mtanyang'anywa tu- Lukuvi
LIVE IKULU: Rais Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara leo Juni 7, 2019

Comments

comments