Baada ya kuikosoa vikali albam ya Jay Z ‘4:44’, 50 Cent ametangaza kuonesha mfano kwa vitendo kwa kuachia albam mpya mwishoni mwa mwaka huu akitamba kuwa itaipiku ya Jigga.

Kiongozi huyo wa G-Unit ambaye hajaachia albam rasmi tangu mwaka 2014 alipoachia ‘Animal Ambition’, amedai kuwa albam hiyo itakuwa na ladha bora zaidi na inayowapa shangwe mashabiki tofauti ya 4:44 ambayo alidai ina lugha ya kisomi na kwamba ni muziki wa kwenye uwanja wa golf.

Wakati 50 Cent anaichana 4:44, Jigga ameendelea kuweka rekodi kubwa na albam hiyo akifika mauzo ya ‘Platinum’ ndani ya wiki chache.

“Nina albam ambayo nilikuwa nasubiri kuiachia,” 50 alifunguka kwenye kipindi cha Access Hollywood Live.

“Itatoka mwishoni mwa mwaka huu. Haitakuwa ‘smart’ kama ya Jay Z. Nataka kufanya muziki ambao watu wakiusikiliza wanapata shangwe. Huwezi kuupata haraka hadi ukae chini uchambue,” alitamba.

Ingawa 50 Cent hakuweka wazi jina la albam hiyo, huenda ikawa ni ‘Street Kings Immortal’ (SKI), jina la mradi aliowahi kuupigia debe tangu mwaka 2012.

Mwaka jana Fiddy aliwahi kusema kwenye moja kati ya mahojiano yake kuwa hawezi kufanya mradi mwingine kabla hajaachia SKI.

Lowassa autaka tena urais mwaka 2020
Apandisha mapepo na kuua waumini wawili kwenye ubatizo

Comments

comments