Kiongozi wa G-Unit, 50 Cent amekerwa na kitendo cha aliyekuwa mpenzi wake, Vivica Fox kuelezea kwenye kitabu chake kipya, maisha yao ya mapenzi na yale waliyofanya faragha.

Fox ameweka kwenye kitabu chake cha ‘Ever Day, I’m Hustling’ jinsi ambavyo alifurahia tendo la ndoa na rapa huyo pamoja na jinsi alivyoweza kumtunza na kumlinda.

Katika kitabu hicho ambacho toleo lake la mtandaoni liliwekwa hivi karibuni, Fox anasimulia, “maisha yetu ya mapenzi yalikuwa mazuri na maalum. Muda mwingi nilikuwa wa kwanza kuomba kufanya tendo la ndoa, kwa sababu nilikuwa nafurahia kuwa naye faragha na kushiriki naye.”

Hata hivyo, 50 hakufurahia hatua hiyo akiita ya kitoto kuweka hadharani mambo yao ya chumbani.

“Nani amefanya huu upuuzi, hii ilikuwa miaka 14 iliyopita,” tafsiri ya maneno makali aliyoandika 50 Cent kwenye Instagram wenye wafuasi milioni 17.4.

Wavamia kituo cha polisi na kuiba baiskeli yao
African Beauty ya Diamond, Ua jekundu la Wema vyazua gumzo mtandaoni