Mahakama ya mwanzo Sinza, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam, imewasomea mashtaka wanawake 40 wakiongozwa na Anger Joseph (22), kwa tuhuma za kufanya biashara ya kuuza miili yao Sinza na Kijitonyama.

Wakisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Winifrida Kayombo, Mwendesha mashtaka Gracy Mwakapesa alidai washtakiwa hao walitenda kosa hilo April 26, saa 2 usiku katika maeneo hayo ya jiji la Dar es salaam.

Na kuwataja baadhi ya wanawake waliokamatwa ni Amina Abdulrahman (25), Sarafina Godfrey (27), Nasra Ismail (22), Anna (19), Modesta Kenned (29), Lilian Mathias(29), Doreen Waziri (18), Rose Fadhili, Jenifer Berege na wengine 30.

Alidai kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kupitia kituo cha polisi cha kijitonyama chini ya Kamanda wa polisi, Shamila Mkonwa.

Washtakiwa wote walikana mashtaka hayo, ambapo dhamana yao ipo wazi, walihitaji kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, watakao saini ahadi ya dhamana ya sh 500,000.

Kesi yao imeahirishwa na kutarajiwa kutajwa tena Mei 13, mwaka huu katika Mahakama hiyo iliyopo Sinza.

Habari Picha: kutoka kwenye maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi jijini Mbeya
JPM awataka wafanyakazi kuwa wavumilivu, 'mishahara itapanda'

Comments

comments