Watu 66 wamefariki dunia katika mlipuko wa bomba la mafuta nchini Mexico na wengine 71 kujeruhiwa vibaya.

Na miongo mwa waliyofariki ni mwanamke mmoja na mtoto wa miaka 12, alisema gavana wa jimbo la Hidalgo, Omar Fayad.

Mlipuko huo ulitokea baada ya bomba hilo kuharibiwa na watu wanaoshukiwa kuwa wezi wa mafuta katika mji wa Tlahuelilpan, jimbo la Hidalgo.

Maafisa wanasema mamia ya watu walikua waking’angania kuchota mafuta kabla ya moto kuzuka ghafla.

Wakazi waliojawa na majonzi bado wamefurika eneo la mkasa huo huku maafisa na wataalamu wa uchunguzi wa maiti wakiendelea kupiga picha maiti zilizotapakaa kila mahali.

Serikali imesema wizi wa mafuta umeigharimu taifa hilo karibu dola bilioni tatu mwaka jana.

Rais Andrés Manuel López Obrador, ambaye aliingia madarakani mwezi Disemba amezindua msako mkali dhidi ya wahalifu hao.

Video: UVCCM wawavaa Zitto na Fatma Karume
Nandy afanya ngoma mpya na Mr.Blue, Tazama