Uzuri wa Tanzania umeendelea kujidhihirisha baada ya mbuga zake tatu kutajwa kuwa moja kati ya mbuga bora zaidi za kutembelea barani Afrika mwaka 2018.

Taasisi ya Safari Bookings iliyofanya tathmini ya kina kubaini mbuga bora zaidi za kutembelea barani Afrika ambapo imetaja Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mbuga za wanyama za Selous na Ngorongoro kuwa maeneo bora zaidi barani Afrika.

Taasisi hiyo iliipa Serengeti alama 4.9 kati ya alama 5 na hivyo kushika nafasi ya kwanza kwenye tathmini hiyo, ikiwa ni mbuga ya pili kwa ukubwa nchini na kongwe zaidi.

Serengeti pia iliwahi kushika nafasi ya kwanza mwaka 2015, mwaka ambao taasisi ya Safari Bookings ilifanya tathmini yake ya mwisho kabla ya iliyofanyika mwaka huu.

Nafasi ya pili [wakati huo] ilishikiliwa na Mbuga ya wanyama ya Mala Mala ya Afrika Kusini ikifuatiwa na Mana Pools ya Zimbabwe.

Serikali imekuwa ikihamasisha utalii wa ndani huku ikihimiza amani na utulivu katika kuendelea kuifanya Tanzania kuwa kisiwa cha amani. Watalii wengi wakiwemo watu maarufu duniani kama wanamuziki mfano Justin Timberlake na wanasoka kama David Bekham.

Peter Schmeichel amtetea Ben Youssef wa Tunisia
TFF kushirikiana na 'La Liga' kuinua soka nchini

Comments

comments