Kiungo Claudio Marchisio anapewa nafasi kubwa ya kujiunga na FC Porto ama SL Benfica zote za nchini Ureno, baada ya kuachana na mabingwa wa soka wa Italia Juventus FC, mwanzoni mwa mwezi huu.

Marchisio mwenye umri wa miaka 32, anapewa nafasi hiyo kutokana na huduma yake ya kusakata soka kuhitajika katika moja ya klabu hizo nguli nchini Ureno, na mpaka sasa haijathibitika ni wapo panapomvutia.

Taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya Ureno zinaeleza kuwa, Marchisio  ana mpango wa kufanya mazungumzo na uongozi wa FC Porto juma hili, na kama ataridhika atajiunga na mabingwa hao wa Ureno.

Lakini taarifa nyingine zimeongeza kuwa huenda uongozi wa SL Benfica ukaingia kati mpango huo na kulazimisha kukutana kwanza na Marchisio, ili kutimiza malengo waliyojiwekea kwa mchezaji huyo, ambaye anahitaji kuhamia nchini Ureno na familia yake.

Kabla ya manguli hao kutajwa kuwa katika vita ya kumuwania kiungo huyo, awali klabu ya Sporting CP (Sporting Lisbon) ilionyesha nia ya kutaka kumsajili, lakini taarifa za mpango huo zilififia na kupotea kabisa.

Marchisio ameeondoka Juventus huku akiwa amecheza michezo 389 tangu mwaka 2006, na amekua mchezaji aliyeiwezesha klabu hiyo kutwaa mataji saba mfululizo ya ligi ya nchini Italia (Serie A).

Sababu kubwa ya kuondoka Allianz Stadium, ilitokana na kukabiliwa na mtihani wa majeraha ya mara kwa mara, hali ambayo ilimnyima kucheza katika kikosi cha kwanza.

Maisha yava vitu 7
Mgombea mmoja wa Udiwani aenguliwa