Takribani watu 95 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na kimbunga cha vumbi kilichopiga kaskazini mwa majiji ya Uttar Pradesh na Rajasthan nchini India.

Kimbunga hicho kilichoripotiwa kutokea jana, kiliharibu miundombinu ya umeme, kiling’oa miti, kuangusha nyumba na kuua watu pamoja na mifugo.

Idadi kubwa zaidi kati ya walioripotiwa kupoteza maisha walikuwa wamelala nyumbani kwao wakati kimbunga hicho kilipokuwa kikivuma.

 

Ingawa hali ya vumbi na upepo katika eneo hili la India hususan wakati wa majira ya joto, idadi kubwa ya vifo iliyoripotiwa  sio jambo la kawaida kwa eneo hilo.

Taarifa zilizotolewa na vyombo vya Serikali ya India zinasema kuwa kati ya waliopoteza maisha, 64 ni kutoka katika jiji la Uttar Pradesh.

Maafisa wa hali ya hewa wametahadharisha kuwa huenda idadi ya wanaopoteza maisha ikaongezeka kutokana hali halisi ya hewa.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi ametumia mtandao wa Twitter kutoa salamu zake za rambirambi na pole kwa wahanga wa kimbunga hicho.

Marco Verratti kufanyiwa upasuaji
AFC yapewa point dhidi ya African Sports

Comments

comments