Jeshi la polisi kikosi cha Usalama barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam limekusanya shilingi 972.7 milioni za makosa ya usalama barabarani katika kipindi cha wiki mbili.

Katika operesheni hiyo ya ukamataji wa magari iliyofanyika kati ya Mei 11 hadi Mei 24 mwaka huu ambapo magari yaliyokamatwa ni 24,116, pikipiki 763, na daladala 10,301.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, kamanda wa kanda hiyo Lazaro Mambosasa alisema.

” Waendesha bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu na kupakia mishikaki yaani abiria zaidi ya mmoja ni 59, jumla ya makosa yaliyokamatwa ni 30,850 na fedha zilizopatikana ni Sh972 milioni.

Ameongezea kuwa madereva na wamiliki wa magari wanatakiwa kulipa faini zao ndani ya siku saba ili kuepuka faini kuongezeka na kusababisha kukamatwa tena kwa kulimbikiza madeni.

 

Video: Jinsi Bale alivyosherekea ushindi na mashabiki Madrid
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Denmark