Mamlaka nchini Uganda, zimewataka wafanyabiashara kujiweka sawa kukabiliana na “wiki ngumu” wakati Kenya ikielekea kwenye uchaguzi mkuu Ugosti 9, 2022 ambayo ndiyo njia kuu ya kusafirisha bidhaa.

Kwa mujibu wa gazeti la The East African, wafanyabiashara wameshauriwa kuchukua tahadhari, ama kuchelewa kuagiza bidhaa au kutumia njia mbadala ya kati Central Corridor licha ya kutokuwepo kwa ushahidi wa kuaminika wa tishio la usalama.

Aidha, Uganda pia imewashauri raia wake wanaoishi na kufanya kazi nchini Kenya, kuchukua tahadhari baada ya Marekani kutoa ilani ya kusafiri kwa wale wanaotembelea mji wa Kisumu.

Hata hivyo, hatua hiyo imekuja wakati Rais Uhuru Kenyatta na maafisa wake wakiuhakikishia umma kuwa uchaguzi huo utakuwa wa amani, huku wagombea wa juu wa urais William Ruto na Raila Odinga nao wakiahidi amani na kukubali kushindwa, iwapo upigaji kura utakuwa huru na wa haki.

Wakati akihutubia Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha mwezi uliopita, Rais Kenyatta alisema, ”hakuna kitakacho haribika.”

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Fred Matiang’i pia amesema vyombo vya usalama vimeimarishwa ili kuhakikisha usalama katika uchaguzi na nchi unakuwa wa uhakika.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Henry Okello Oryem amesema wanatarajia uchaguzi wa Kenya utamalizika kwa amani lakini Uganda inajiandaa na hali yoyote itakayojitokeza.

Amesema, ”ikiwa na mpango B wa kuwa na akiba ya bidhaa muhimu kama litatokea lolote basi tutabadilisha njia usafarishaji bidhaa kwa kupitia Tanzania.”

Profesa afunga hesabu za uchaguzi na harakati za Bangi

Mfahamu mwanasiasa mkongwe nchini Kenya Raila Amolo Odinga
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo August 7, 2022