Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili na kukagua Vikundi vya Wajasiriamali katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika Visiwani Zanzibar.

Rais Dkt. Hussein Mwinyi, ni Mgeni Rasmi na mdau wa lugha ya Kiswahili katika kilele cha maadhimisho haya, na zifuatazo ni picha zinazomuonesha akikagua mabanda mbalimbali ya wanasiriamali katika eneo la Hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika banda la moja ya wajasiriamali katika siku ya maadhimisho ya Kiswahili Duniani yanayofanyika hii leo Julai 7, 2022 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipokea zawadi katika moja ya banda la vitabu vya Kiswahili la wajasiriamali hii leo Julai 7, 2022 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipata maelekezo toka kwa wajasiriamali wa mazulia na mifagio ikiwa ni siku ya maadhimisho ya Kiswahili Duniani yanayofanyika hii leo Julai 7, 2022 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisoma kipeperushi mara baada ya kuwasili eneo la viwanja vya Hotel ya Golden Tulip hii leo Julai 7, 2022 Visiwani Zanzibar.

Kocha Mtibwa Sugar afichua siri ya kuing'oa Tanzania Prisons
Kiswahili chaundiwa mikakati kuiteka Dunia