Kamati ya usimamizi na uendeshaji (Kamati ya saa 72) imempa adhabu ya Kumfungia miezi mitatu Katibu Mkuu wa klabu bya Rhino Rangers, Dickson Cyprian Mgalike kwa kosa la kuidanganya kamati hiyo kwa kutoa taarifa potofu katika barua aliyoiandikia Bodi ya Ligi.

Hapo awali, Kamati ilimuadhibu Mchezaji Sameer Mwinyishere kwa kosa la kumrushia chupa ya maji mwamuzi.

Katibu Dickson Cyprian Mgalike, aliandika barua iliyoeleza kuwa, Sameer hakufanya kosa hilo na alimtaja mchezaji Yusuf Mputa kwamba ndiye aliyefanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kumrushia Mwamuzi chupa ya maji.

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji kwa kushirikiana watendaji wa Bodi ya Ligi ilifanya uchunguzi na kubaini mchezaji Yusuph Mputa hakuwepo kwenye Orodha ya Wachezaji wa siku hiyo.  Adhabu hiyo imetolewa kwa kufuata kanuni ya 41(6).

Safari Ya Kuijenga Serengeti Boys Mpya Kuanza Kesho
Azam FC Yachomoza Hispania