Kijana mwenye umri wa miaka 24, Mohamed Nufal, raia wa Misri jana alianza rasmi safari yake kutoka jijini Cairo akielekea nchini Urusi kwa lengo la kushuhudia fainali za kombe la dunia.

Nufal ambaye ameanza safari yake leo katika eneo la Tahrir Square na anatarajia kuendesha baiskeli hiyo kwa umbali wa kilometa 5,000 kwa muda wa siku 65 akiwa barabarani.

Lengo la Nufal ni kuhakikisha anashuhudia mechi ya kwanza ya Misri jijini Moscow ikiwa ni mara ya kwanza kwa taifa hilo kushiriki fainali hizo tangu miaka 28 iliyopita.

Katika safari yake, amepanga kupitia Jordan, Bulgaria, Romania, Moldova na Ukraine. Hata hivyo, atalazimika kupanda ndege kuvuka Syria kutokana na vita inayoendelea katika nchi hiyo. Atapita angani Iraq  kwa sababu za kiusalama, na kisha kuendelea na safari yake kwa baiskeli barabarani.

Katika safari yake, atabeba spea za baiskeli, simu kadhaa kwa ajili ya mawasiliano na hema. Mbali na kulala kwenye mahoteli atakayokuwa amefika kwenye miji kadhaa anategemea ukarimu wa watu asiowafahamu atakaokutana nao katika safari yake.

“Ni kupata uzoefu wa barabara zaidi hata ya kushuhudia Kombe la Dunia. Ingekuwa Kombe la Dunia ndio nia pekee, ningeweza kupanda ndege. Lakini nataka kuona vitu vipya,” Nufal aliiambia Reuters.

Baadhi ya marafiki wa karibu Nufal walikusanyika kumsindikiza akianza safari yake.

Magazeti ya nje na ndani ya Tanzania leo Aprili 9, 2018
Video: Dar24 Media yatoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya