Msanii Abby Chams kutoka Tanzania ametembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai ambapo alipokelewa na Kamishna Jenerali wa Banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai Balozi Mohammed Abdallah Mtonga na Mkurugenzi wa Banda la Tanzania Getrude Ng’weshemi kutoka TanTrade pamoja na wawakilishi wa Sekta mbalimbali zinazoshiriki kwenye maonesho haya.

Baada ya kupokelewa Abby Chams alitembezwa kwenye banda la Tanzania akiongozwa na Mkurugenzi wa Banda kujionea mambo mbalimbali yaliyopo kwenye banda na kujifunza namna ambavyo Tanzania imetumia fursa ya ushiriki kwenye maonesho haya ya Expo 2020 Dubai kutangaza upekee wake, vivutio mbalimbali na fursa kubwa zilizopo nchini.

Ndani ya banda la Tanzania muonekano wa maudhui wake umesheheni maudhui mbalimbali yanayoitangaza Tanzania kupitia sekta mbalimbali zilizopewa kipaumbele ambazo ni Utalii, Madini, Kilimo, Miundombinu na Miradi mikubwa ya kimkakati.

Msanii Abby Chams akitembelea eneo la Tanzanite

Zoezi hili la kutembelea banda la Tanzania lilienda sambamba na tukio maalum lililoandaliwa kwa msanii Abby Chams ambapo balozi Mtonga alimkaribisha Abby Chams kwenye eneo ambalo yanaonyeshwa madini ya ‘Tanzanite’.

Balozi Mtonga alisema,”fursa aliyoipata Abby Chams kutembelea katika banda letu leo akiwa kama kijana ambaye ameiwakilisha vema Tanzania hapa kwenye maonesho haya ya Expo 2020 napenda kutumia nafasi hii ya uwepo wake kama alama ya kufungua rasmi eneo la ‘Tanzanite’ kwenye banda letu ambapo tutakuwa tunauonesha Ulimwengu upekee wake ili waweze kuja kujifunza na kujionea dhahiri sio tu wabaki kuisikia.

Kwa upekee wake madini haya yanapatikana Tanzania peke yake kote ulimwenguni. Kupitia zoezi hili pia ninafungua rasmi duka la kuuza ‘Tanzanite’ ndani ya banda la Tanzania ambalo litauza vito mbalimbali vya thamani katika maonesho ya Expo 2020 Dubai kupitia kampuni ya The Tanzanite Experience kutoka Tanzania inayojishuhulisha na uuzaji wa vito vya thamani vya ‘Tanzanite’ na kuielimisha jamii

Mosimane amkingia kifua Luis Miquissone
Mchele wa Morogoro kuuzwa kimataifa