Baada ya kuthibitika Kocha kutoka nchini Kenya Patrick Odhiambo amesitishiwa ajira yake huko Tanzania Prisons kufuatia kupoteza dhidi ya Ihefu FC, Jumamosi (Januari 26), Kocha wa Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi 2023 Mlandege FC Abdallah Bares ‘Arteta’.

Tanzania Prisons imekua na matokeo mabaya kwa michezo kadhaa ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ambapo hadi sasa imejikusanyia alama 21, ikishika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi hiyo yenye timu 16.

Bares anatajwa kuwa kwenye mpango wa kutangazwa kuwa Kocha Mkuu Klabuni hapo, kutokana na uwezo na uzoefu wake katika Soka la Tanzania Bara, akizinoa klabu za JKT Tanzania, Polisi Tanzania na Tanzania Prisons.

Katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023, Bares aliiongoza Mlandege FC kwa kupata ushindi michezo mitatu, huku akiambulia sare moja.

Mwili wa Mwandishi aliyetoweka wakutwa nje ya jiji
Simba SC yarejea Dar, wachezaji wapewa mapumziko