Kocha mkuu wa Wekundu Wa Msimba Simba, Jackson Mayanja amekunjua makucha ya kuhitaji nidhamu kikosini mwake, baada ya kumuweka pembeni Abdi Banda, ambaye anadaiwa kugomea maagizo ya kocha huyo.

Abdi Banda anadaiwa kuonesha utovu wa nidhamu, wakati wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga, baada ya kutakiwa kupasha misuli jito kabla ya kuingia uwanjani kuongeza nguvu.

Banda aligomea agizo hilo la Mayanja, huku akihoji kwa nini asianze tangu mwanzo wa mchezo huo, na badala yake anaanzia benchi, kitendo ambacho alichokitafsiri kama kutoaminiwa na kocha wake.

Abdi Banda ni mtoto wa beki wa zamani wa Simba Hassan Abdi Banda, ambaye alikuwa na nidhamu ya hali ya juu miongoni mwa wachezaji  waliounda kikosi cha Msimbazi kwa wakati huo.

“Mimi kama kocha wa Simba naweza kumpangia mchezaji chochote cha kufanya kwa kuwa kazi iliyomleta kikosini ni kucheza mpira, sasa nashangaa anakataa agizo langu? tena mbele ya watazamaji! hivi mimi na yeye nani yupo juu ya mwenzake?

“Nasema hivi mchezaji amesaini mkataba wa kufanya kazi ya kucheza mpira kwenye klabu na kama hataki kutimiza wajibu wake kwangu hana nafasi hata kidogo, mimi siwezi kumbembeleza wakati anajua wajibu wake” Alisema Mayanja.

Mayanja ameongeza kuwa anamshangaa Banda kugomea maelekezo yake, wakati wachezaji wengine kikosini mwake wana nidhamu ya kutosha na hufuata kile anachowaelekeza.

Hata hivyo alipoulizwa kama adhabu gani atakayompa Banda kutokana na kitendo hicho, Mayanja alisema kamati ya nidhamu ya Simba ndiyo yenye jukumu la kuamua adhabu gani anayostahili kwa kile alichokifanya.

Banda anakua mchezaji wa pili kuingia katika mtego wa utovu wa nidhamu

akitokea Costal Union, akitanguliwa na Hassan Isihaka ambaye anatumikia adhabu ya kutocheza kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Chris Coleman: Ni Marufuku Wachezaji Kusafiri Na Wake Zao
Joe Hart Na Raheem Sterling Waondolewa Timu Ya Taifa