Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini TFF imemfungia michezo miwili beki wa Simba, Abdi Banda kwa kosa la kumpiga ngumi, kiungo na nahodha wa Kagera Sugar George Kavilla, wakati wa mchezo wa ligi kuu uliochezwa  Aprili 2 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Hatua hiyo inamaanisha Banda yupo huru kuendelea kuichezea Simba, kwani tayari ameshakosa michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC timu yake ikishinda 3-2 na kisha mchezo dhidi ya Toto Africans ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kabla ya kufikishwa mbele ya kamati ya nidhamu, Banda alimuomba radhi nahodha wa Kagera Sugar George Kavila, kwa kitendo alichomfanyia, na pia aliwataka wadau wa soka nchini kumsamehe kwa tukio hili ambalo halikuonwa na mwamuzi.

Picha za televisheni zilionyesha Banda akitenda kosa la kumpiga Kavila, na ndipo taratibu nyingine za kinidhamu zikaanza kuchukuliwa dhidi ya beki huyo.

Ligi Kuu Kuendelea Shinyanga
Opinions of Custom Writing Service with respect to School students