Ali kiba ambaye siku ya alhamisi ya tarehe 19, April, 2018 alifunga ndoa na binti Aminah Rikesh kutoka nchini Kenya katika mji wa Mombasa, ambapo inatarajiwa Ali kiba kuirudisha sherehe hiyo nyumbani Tanzania tarehe 29. Siku hiyo Ali kiba aliweka wazi mdogo wake Abdu kiba kuwa ataoa karibuni.

Ahadi hiyo ya Ali kiba kuhusu mdogo wake imetimia kwani msanii huyo ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ya ‘Jeraha’ amefunga ndoa pia na moja ya mtu wake wa karibu na kufanikiwa kuongeza idadi ya wanawake katika familia yao kama ambavyo mdogo wake wa kike Zabibu alivyosema kuwa mwanzo walikuwa wawili tu yeye na mama yake lakini ameongezeka mke wa Kiba na kudai anatarajia kuongezeka mwingine wa nne karibuni ambae ndiye mke wa Abdu kiba.

Kwa upande wake msanii anayejulikana kwa jina la H Baba ambaye ni mtu wa karibu na kina Ali kiba ameweka wazi kuwa Abdu kiba leo amefunguka ndoa na kumtakia kheri kwenye siku yake hiyo muhimu katika maisha yake.

“Hongera sana Abdu Kiba kwa kuchukua jiko lako Allah akulindie ndoa yako, jambo la kheri uja na kheri zake karibu chama la waliompendeza Mungu kwani kuoa ni jambo la kheri,”ameandika H Baba

Hata hivyo, Ali kiba na Abdu Kiba wanadhaniwa kuwa huenda wanaweza kufanya sherehe ya pamoja April 29, 2018 jijini Dar es Salaam ili kufurahi na watu wao wa karibu kufuatia zoezi lao la kufunga ndoa.

ACT yasitisha mkutano kwa sababu za kiusalama
Polepole akemea wanaomchafua Rais

Comments

comments