Msanii Abdu Kiba ambaye ni mdogo wake Ali Kiba amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz.

Ali Kiba na Diamond Platinumz ni washindani wakuu nchini huku taswira inayoonesha na mashabiki wao hususan waliounda timu inaonesha uhasimu kati ya wasanii hao. Ingawa kila wanapoulizwa hueleza kuwa hawana tofauti, picha inaeleza tofauti.

Abdu Kiba ambaye hivi karibuni ameachia video yake ya ‘Bayoyo’, ameiambia Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa endapo atawekewa pesa ya kutosha mezani yuko tayari kufanya kazi na lebo hiyo.

“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,” aliongeza.

Video: Watumishi hewa wa bungeni kupoteza milioni 40 kwa siku
Kenya: Tumbili azima umeme Nchi Nzima